Jumatatu 16 Juni 2025 - 22:57
Natamani nami ningelikuwa Muirani

Hawza/ "Monaem", mwanafunzi wa udaktari kutoka Palestina, aliandika katika ukurasa wake wa mitandao ya kijamii: Heri yenu… Leo ninatamka kutoka moyoni: Laiti ningelikuwa mimi pia Muirani, ili niwe mshirika katika adhama na heshima hii ambayo mataifa tele duniani yanajivunia.

Kwa mujibu wa Idara ya Habari ya Kimataifa ya Shirika la Habari la Hawza, mashambulizi makubwa na ya kushtukiza yaliyofanywa na Iran dhidi ya ardhi zilizokaliwa kwa mabavu, kwa kujibu uhalifu uliofanya na utawala huo siku ya Ijumaa iliyopita na kuwaua mashahidi kadhaa miongoni mwa makamanda wa kijeshi, wanasayansi na raia wasio na hatia, yamepata mwitiko mkubwa katika nyanja za kisiasa na vyombo vya habari duniani kote. Katika mazingira haya, watu kutoka mataifa mbalimbali, Waislamu na wanaozungumza Kiarabu, vijana kutoka nchi za Ghuba, watu wa Ghaza, na vijana wa Lebanon na Yemen, wameonyesha hisia zao kuhusu ushindi huu mkubwa. Wametoa shukrani kwa Jeshi la ulinzi la Mapinduzi na kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi kutokana na nguvu hii ya kushangaza, na wametaka kuendelezwa kwa hamasa hii kubwa hadi kufikia hatua ya kuuangamiza kikamilifu utawala wa Kizayuni.

Katika muktadha huu, Muhammad Monaem, mwanafunzi anaesomea udaktari wa Kipalestina, ameandika ujumb wakee wa moyoni uliowalenga watu wa Iran:

Enyi watu wapendwa na wenye heshima wa Iran, msidanganyike na maneno ya maadui na walaghai hawa. Endeleeni kusimama imara nyuma ya nchi yenu na taifa lenu, kama mlivyokuwa daima. Mnaishi katika ardhi ambayo katika ulimwengu mzima inaelezea maana ya wivu, ushujaa, heshima, na kusimama kidete. Ninyi ndio taifa pekee lililoweza kusimama dhidi ya uhalifu wa mabeberu na kuwapa pigo kali wauaji hao.

Inatosha tu kuangalia kwenye mitandao ya kijamii, ili kuona ni jinsi gani vijana kutoka Ulaya, Asia, Afrika, na hata Marekani walivyo upande wenu; jinsi wanavyopaza sauti kwa fahari jina la Iran na kuwaombea askari wa Kiirani.

Heri yenu… Leo ninatamka kutoka moyoni: Laiti ningelikuwa mimi pia Muirani, ili niwe mshirika katika adhama na heshima hii ambayo mataifa tele ulimwengubi yanajivunia. Wazayuni wanaogopa maendeleo ya taifa hili la kale, na wanadhani wanaweza kusimama mbele ya historia yenu ya miaka elfu saba... lakini wako katika makosa makubwa.

Ustaarabu wa Iran, kama daima, umeathiri dunia nzima, na wivu wa kishujaa wa Muirani umekuwa sifa maarufu ulimwenguni. Mamilioni ya watu huru duniani wako tayari kupigana bega kwa bega nanyi, na kuwatolea vijana wao kafara kwa ajili ya Iran.

Mimi, Mpalestina ambaye kwa miaka mingi nimekuwa mgeni katika ardhi hii tukufu, leo ninatamka kwa dhati ya moyo wangu: Nafsi yangu naitoa Iran. Niko tayari kujitolea kulilinda taifa hili lenye heshima na ardhi hii takatifu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha